Yoeli 1:17-20 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Mbegu zinaoza udongoni;ghala za nafaka ni ukiwa mtupu,ghala zimeharibika,kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.

18. Tazama wanyama wanavyolia kwa huzuni!Makundi ya ng'ombe yanahangaika,kwa sababu yamekosa malisho;hata makundi ya kondoo yanateseka.

19. Ninakulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu,moto umemaliza malisho nyikani,miali ya moto imeteketeza miti mashambani.

20. Hata wanyama wa porini wanakulilia wewe,maana, vijito vya maji vimekauka,moto umemaliza malisho nyikani.

Yoeli 1