3. Hupinda maneno yao kama pinde;wameimarika kwa uongo na si kwa haki.Huendelea kutoka uovu hata uovu,wala hawanitambui mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
4. Kila mmoja ajihadhari na jirani yake!Hata ndugu yeyote haaminiki,kila ndugu ni mdanganyifu,na kila jirani ni msengenyaji.
5. Kila mmoja humdanganya jirani yake,hakuna hata mmoja asemaye ukweli.Wamezifundisha ndimi zao kusema uongo;hutenda uovu kiasi cha kushindwa kabisa kutubu.
6. Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma,na udanganyifu juu ya udanganyifu.Wanakataa kunitambua mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?
8. Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu,daima haziishi kudanganya;kila mmoja huongea vema na jirani yake,lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.