1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni,dhidi ya wakazi wa Kaldayo.
2. Nitawapeleka wapepetaji Babuloni,nao watampepeta;watamaliza kila kitu katika nchi yakewatakapofika kuishambulia toka kila upandewakati wa maangamizi yake.”
3. Usiwape nafasi wapiga mshale wa Babuloni;usiwaache wavute upinde,wala kuvaa mavazi yao ya vita.Usiwahurumie vijana wake;liangamize kabisa jeshi lake.
4. Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo,watajeruhiwa katika barabara zake.
5. Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi,ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli.