Yeremia 50:27-33 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Waueni askari wake hodari;waache washukie machinjoni.Ole wao, maana siku yao imewadia,wakati wao wa kuadhibiwa umefika.

28. “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

29. “Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.

30. Kwa hiyo, vijana wake watauawa katika mitaa yake, na majeshi yake yote yataangamizwa siku hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

31. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,napigana nawe ewe mwenye kiburi,maana siku yako ya adhabu imefika,wakati nitakapokuadhibu umewadia.

32. Mwenye kiburi atajikwaa na kuanguka,wala hapatakuwa na mtu wa kumwinua.Nitawasha moto katika miji yake,nao utateketeza kila kitu kandokando yake.”

33. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Watu wa Israeli wanakandamizwa; hali kadhalika na watu wa Yuda. Wale waliowachukua mateka wamewabana sana na wanakataa kuwaachia.

Yeremia 50