13. Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
14. Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu,mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa:“Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu;inukeni mwende kuushambulia!
15. Mimi Mwenyezi-Mungu nitakufanya wee Edomukuwa mdogo kuliko mataifa yote.Ulimwengu wote utakudharau.
16. Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya,ewe ukaaye katika mapango ya miamba,unayeishi juu ya kilele cha mlima!Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai,mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
17. “Edomu itakuwa kitisho na kila mtu atakayepita karibu yake atashangaa, na kuizomea kwa sababu ya maafa yatakayoipata.
18. Kama vile Sodoma na Gomora na miji jirani yake ilivyoangamizwa, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, hakutakuwa na mtu yeyote atakayeishi Edomu wala kufanya mashauri humo.