1. Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Yeremia kuhusu watu wa mataifa.
2. Kuhusu Misri na jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililokuwa huko Karkemishi karibu na mto Eufrate ambalo Nebukadneza mfalme wa Babuloni alilishambulia mnamo mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
3. Tayarisheni ngao ndogo na kubwamsonge mbele kupigana vita.
4. Tandikeni farasi na kuwapanda,Shikeni nafasi zenu na kofia za chuma mvae.Noeni mikuki yenu,vaeni mavazi yenu ya chuma!
5. Lakini mbona nawaona wametishwa?Wamerudi nyuma.Mashujaa wao wamepigwa,wamekimbia mbio,bila hata kugeuka nyuma.Kitisho kila upande.Mwenyezi-Mungu amesema.
6. Walio wepesi kutoroka hawawezi,mashujaa hawawezi kukwepa;huko kaskazini kwenye mto Eufratewamejikwaa na kuanguka.
7. Nani huyo aliye kama mto Nili uliofurikakama mito inayoumuka mawimbi?
8. Misri ni kama mto Nili uliofurikakama mito inayoumuka mawimbiIlisema: “Nitajaa, nitaifunika nchi,nitaiharibu miji na wakazi wake.
9. Songeni mbele, enyi farasi,shambulieni enyi magari ya farasi.Mashujaa wasonge mbele:Watu wa Kushi na Puti washikao ngao,watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”