10. Kisha nikasema: “Aa, Mwenyezi-Mungu, hakika umewadanganya kabisa watu hawa na mji wa Yerusalemu! Uliwaambia mambo yatawaendea vema, kumbe maisha yao yamo hatarini kabisa!”
11. Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na mji wa Yerusalemu, “Upepo wa hari kutoka vilele vikavu vya jangwani utawavumia watu wangu. Huo si upepo wa kupepeta au kusafisha,
12. bali ni upepo mkali sana utokao kwangu. Ni mimi Mwenyezi-Mungu nitakayetoa hukumu juu yao.”
13. Tazama! Adui anakuja kama mawingu.Magari yake ya vita ni kama kimbunga,na farasi wake waenda kasi kuliko tai.Ole wetu! Tumeangamia!
14. Yerusalemu, yasafishe maovu moyoni mwako,ili upate kuokolewa.Mpaka lini utaendelea kuwaza maovu?
15. Sauti kutoka Dani inatoa taarifa;inatangaza maafa kutoka vilima vya Efraimu.
16. Inayaonya mataifa,inaitangazia Yerusalemu:“Wavamizi waja kutoka nchi ya mbali,wanaitisha miji ya Yuda,
17. wanauzingira Yerusalemu kama walinda mashamba,kwa sababu watu wake wameniasi mimi Mwenyezi-Mungu.
18. Yuda, mwenendo wako na matendo yako yamekuletea hayo.Hayo ndiyo maafa yaliyokupata, tena ni machungu;yamepenya mpaka ndani moyoni mwako.”
19. Uchungu, uchungu!Nagaagaa kwa uchungu!Moyo wangu unanigonga vibaya.Wala siwezi kukaa kimya.Maana naogopa mlio wa tarumbeta,nasikia kingora cha vita.
20. Maafa baada ya maafa,nchi yote imeharibiwa.Ghafla makazi yangu yameharibiwa,na hata mapazia yake kwa dakika moja.