1. Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu:
2. “Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Yaandike katika kitabu maneno yote niliyokuambia.
3. Maana siku zaja ambapo nitawarudishia fanaka zao watu wangu wa Israeli na Yuda na kuwarudisha katika nchi niliyowapa wazee wao, nao wataimiliki. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
4. Haya ndiyo mambo aliyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu watu wa Israeli na Yuda:
5. “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Kumesikika kilio cha hofusauti ya kutisha wala si ya amani.
6. Jiulizeni sasa na kufahamu:Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto?Mbona basi, namwona kila mwanamumeamejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utunguna nyuso zao zimegeuka rangi?
7. Kweli, siku hiyo ni kubwa,hakuna nyingine kama hiyo;ni siku ya huzuni kwa watu wa Yakobo;hata hivyo, wataokolewa humo.
8. “Siku hiyo itakapofika, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitaivunja nira iliyo shingoni mwao na kukata minyororo yao.
9. Nao hawatakuwa tena watumwa wa wageni, bali watanitumikia mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, na mfalme wa ukoo wa Daudi ambaye nitawateulia.