Yeremia 20:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja namikwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha;kwa hiyo watesi wangu watajikwaa,na hawataweza kunishinda.Wataaibika kupindukia,maana hawatafaulu.Fedheha yao itakuwa ya daima;kamwe haitasahaulika.

12. Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,wewe humthibiti mtu mwadilifu,huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu,unijalie kuona ukiwalipiza kisasi,maana kwako nimekiweka kisa changu.

13. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu;msifuni Mwenyezi-Mungu,kwani ameyaokoa maisha ya mhitaji,kutoka mikononi mwa watu waovu.

14. Na ilaaniwe siku niliyozaliwa!Siku hiyo mama aliponizaa,isitakiwe baraka!

15. Na alaaniwe aliyempelekea baba ujumbe:“Umepata mtoto wa kiume”,akamfanya ajae furaha.

16. Mtu huyo na awe kama mijialiyoiangusha Mwenyezi-Mungu bila huruma.Mtu huyo na asikie kilio asubuhi,na mchana kelele za vita,

17. kwani hakuniua tumboni mwa mama yangu;mama yangu angekuwa kaburi langu,tumbo lake lingebaki kubwa daima.

18. Kwa nini nilitoka tumboni mwa mama yangu?Je, nilitoka ili nipate taabu na huzunina kuishi maisha ya aibu?

Yeremia 20