Yeremia 2:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)

35. wewe wasema: ‘Mimi sina hatia;hakika hasira yake imegeuka mbali nami.’Lakini mimi nitakuhukumu kwa sababu unasema:‘Sikutenda dhambi.’

36. Kwa nini unajirahisisha hivi,ukibadilibadili mwenendo wako?Utaaibishwa na Misri,kama ulivyoaibishwa na Ashuru.

37. Na huko pia utatoka,mikono kichwani kwa aibu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimewakataa wale uliowategemea,wala hutafanikiwa kwa msaada wao.

Yeremia 2