Yeremia 18:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Kwa hiyo waache watoto wao wafe njaa,waache wafe vitani kwa upanga.Wake zao wawe tasa na wajane.Waume zao wafe kwa maradhi mabayana vijana wao wachinjwe kwa upanga vitani.

22. Kilio na kisikike majumbani mwao,unapowaletea kundi la wanyanganyi ghafla.Maana wamechimba shimo waninase;wameitegea mitego miguu yangu.

23. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu,wazijua njama zao zote za kuniua.Usiwasamehe uovu wao,wala kufuta dhambi zao.Waanguke chini mbele yako;uwakabili wakati wa hasira yako.

Yeremia 18