15. Havina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati vitakapoadhibiwa vyote vitaangamia.
16. Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo,maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote,na Israeli ni taifa lililo mali yake;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
17. Kusanyeni vitu vyenu enyi watu mliozingirwa.
18. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii,nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
19. Ole wangu mimi Yerusalemu maana nimejeruhiwa!Jeraha langu ni baya sana!Lakini nilisema: “Hakika haya ni mateso,na sina budi kuyavumilia.”
20. Lakini hema langu limebomolewa,kamba zake zote zimekatika;watoto wangu wameniacha, na kwenda zao,wala hawapo tena;hakuna wa kunisimikia tena hema langu,wala wa kunitundikia mapazia yangu.
21. Nami Yeremia nikasema:Wachungaji wamekuwa wajinga,hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu;kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa,na kondoo wao wote wametawanyika.
22. Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia.Kuna kishindo kutoka kaskazini.Taifa kutoka kaskazini linakuja,kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwaambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!