14. Binadamu ni mjinga na mpumbavu;kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake;maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu.Havina uhai wowote ndani yao.
15. Havina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati vitakapoadhibiwa vyote vitaangamia.
16. Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo,maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote,na Israeli ni taifa lililo mali yake;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
17. Kusanyeni vitu vyenu enyi watu mliozingirwa.
18. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii,nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
19. Ole wangu mimi Yerusalemu maana nimejeruhiwa!Jeraha langu ni baya sana!Lakini nilisema: “Hakika haya ni mateso,na sina budi kuyavumilia.”
20. Lakini hema langu limebomolewa,kamba zake zote zimekatika;watoto wangu wameniacha, na kwenda zao,wala hawapo tena;hakuna wa kunisimikia tena hema langu,wala wa kunitundikia mapazia yangu.
21. Nami Yeremia nikasema:Wachungaji wamekuwa wajinga,hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu;kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa,na kondoo wao wote wametawanyika.
22. Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia.Kuna kishindo kutoka kaskazini.Taifa kutoka kaskazini linakuja,kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwaambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!
23. Najua, ee Mwenyezi-Mungu,binadamu hana uwezo na maisha yake;hakuna mtu awezaye kuyaongoza maisha yake.