1. Sikilizeni neno analowaambieni Mwenyezi-Mungu,enyi Waisraeli!
2. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Msijifunze mienendo ya mataifa mengine,wala msishangazwe na ishara za mbinguni;yaacheni mataifa mengine yashangazwe nazo.
3. Maana, mila za dini za watu hawa ni za uongo.Mtu hukata mti msitunifundi akachonga kinyago cha mungu kwa shoka.
4. Kisha watu hukipamba kwa fedha na dhahabuwakakipigilia misumari kwa nyundoili kisije kikaanguka.
5. Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndegekatika shamba la matango,havina uwezo wa kuongea;ni lazima vibebwemaana haviwezi kutembea.Msiviogope vinyago hivyo,maana haviwezi kudhuru,wala haviwezi kutenda lolote jema.”
6. Ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe;wewe ni mkuu na nguvu yako yajulikana.
7. Nani asiyekuogopa wewe, ee mfalme wa mataifa?Wewe wastahili kuheshimiwa.Miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa,na katika falme zao zote,hakuna hata mmoja aliye kama wewe.