Wimbo Ulio Bora 6:9-12 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Hua wangu, mzuri wangu, ni mmoja tu,na ni kipenzi cha mama yake;yeye ni wa pekee kwa mama yake.Wasichana humtazama na kumwita heri,nao malkia na masuria huziimba sifa zake.

10. Nani huyu atazamaye kama pambazuko?Mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,na anatisha kama jeshi lenye bendera.

11. Nimeingia katika bustani ya milozikutazama machipuko ya bondeni,kuona kama mizabibu imechanua,na mikomamanga imechanua maua.

12. Bila kutazamia, mpenzi wangu,akanitia katika gari la mkuu.

Wimbo Ulio Bora 6