Wimbo Ulio Bora 6:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Hebu tazama kando tafadhali;ukinitazama nahangaika.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,wateremkao chini ya milima ya Gileadi.

6. Meno yako kama kundi la kondoo majikewanaoteremka baada ya kuogeshwa.Kila mmoja amezaa mapacha,na hakuna yeyote aliyefiwa.

7. Mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga,nyuma ya shela lako.

8. Wapo malkia sitini, masuria themanini,na wasichana wasiohesabika!

9. Hua wangu, mzuri wangu, ni mmoja tu,na ni kipenzi cha mama yake;yeye ni wa pekee kwa mama yake.Wasichana humtazama na kumwita heri,nao malkia na masuria huziimba sifa zake.

10. Nani huyu atazamaye kama pambazuko?Mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,na anatisha kama jeshi lenye bendera.

11. Nimeingia katika bustani ya milozikutazama machipuko ya bondeni,kuona kama mizabibu imechanua,na mikomamanga imechanua maua.

12. Bila kutazamia, mpenzi wangu,akanitia katika gari la mkuu.

Wimbo Ulio Bora 6