15. Miguu yake ni kama nguzo za alabastazilizosimikwa katika misingi ya dhahabu.Umbo lake ni kama Lebanoni,ni bora kama miti ya mierezi.
16. Kinywa chake kimejaa maneno matamu,kwa ujumla anapendeza.Basi, hivyo ndivyo alivyo mpenzi wangu,naam, ndivyo alivyo rafiki yangu,enyi wanawake wa Yerusalemu.