Walawi 21:15-24 Biblia Habari Njema (BHN)

15. asije akawatia unajisi watoto wake mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyemweka wakfu.”

16. Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

17. “Mwambie Aroni hivi: Mzawa wako yeyote katika vizazi vyote vijavyo ambaye ana dosari mwilini, haruhusiwi kukaribia na kunitolea mimi Mungu wake sadaka ya mkate.

18. Mtu yeyote mwenye dosari sikaribie kunitolea sadaka: Awe kipofu, aliyelemaa, aliyeharibika uso, mwenye kiungo kirefu kuliko kawaida,

19. mwenye mguu au mkono ulioumia,

20. mwenye kibyongo, mtu mfupi kuliko kawaida, mwenye macho mabovu au ugonjwa wa ngozi, mwenye upele au towashi.

21. Mzawa yeyote wa kuhani Aroni mwenye kilema asikaribie kunitolea sadaka za kuteketezwa kwa moto; kwa vile ana kilema, basi, asikaribie kunitolea mimi Mungu mkate wangu.

22. Mtu huyo anaweza kula mkate wa Mungu wake, vitu vitakatifu na vile vitakatifu kabisa.

23. Lakini asilikaribie lile pazia wala ile madhabahu kwani ana dosari, asije akapatia unajisi mahali patakatifu; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ndiye ninayewaweka wakfu.”

24. Mose akamweleza Aroni na wanawe na Waisraeli wote mambo hayo yote.

Walawi 21