Walawi 11:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu aliwaambia Mose na Aroni,

2. “Wawaambie Waisraeli hivi:

3. Kati ya wanyama wote duniani, mmeruhusiwa kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

4. Lakini msile mnyama yeyote ambaye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili, au ambaye kwato zake zimegawanyika lakini hacheui. Msile ngamia, kwani hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili. Kwenu huyo ni najisi.

5. Pelele msimle; yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi.

6. Sungura msimle; yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi.

7. Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi.

8. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.

9. “Samaki yeyote wa baharini au mtoni mwenye mapezi na magamba, mnaweza kumla.

10. Lakini chochote kinachoishi baharini au mitoni, ambacho hakina mapezi wala magamba, yaani viumbe vyote viendavyo majini na viumbe vingine vyote viishivyo majini ni najisi kwenu.

11. Viumbe hivyo vitakuwa daima najisi kwenu. Msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao kwani ni najisi.

Walawi 11