Waebrania 8:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kama yeye angekuwa wa hapa duniani, asingekuwa kamwe kuhani, kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na sheria.

5. Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”

6. Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.

7. Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili.

Waebrania 8