Waebrania 8:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: Sisi tunaye kuhani mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mkuu mbinguni.

2. Yeye hutoa huduma ya kuhani mkuu mahali patakatifu katika maskani, yaani ndani ya ile hema ya kweli iliyojengwa na Bwana, siyo na binadamu.

3. Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea.

4. Kama yeye angekuwa wa hapa duniani, asingekuwa kamwe kuhani, kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na sheria.

5. Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”

Waebrania 8