Waebrania 10:31-39 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!

32. Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, nyinyi mlistahimili.

33. Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo.

34. Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.

35. Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa.

36. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi.

37. Maana kama yasemavyo Maandiko:“Bado kidogo tu,na yule anayekuja, atakuja,wala hatakawia.

38. Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi;walakini akirudi nyuma,mimi sitapendezwa naye.”

39. Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.

Waebrania 10