Ufunuo 3:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika:“Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!

2. Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.

3. Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii na kutubu. Usipokesha nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutaijua saa nitakapokujia.

4. Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wamevaa mavazi meupe.

5. “Mshindi atavikwa hivyo kwa mavazi meupe. Nami sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uhai; tena nitamkiri kwamba ni wangu mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika wake.

6. “Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!

7. “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi:“Mimi niliye mtakatifu na wa kweli, ambaye nina ule ufunguo wa Daudi na ambaye hufungua na hakuna awezaye kufunga, hufunga na hakuna awezaye kufungua.

Ufunuo 3