1. Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu,
2. kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi,kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu,kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
3. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu enyi wanyenyekevu wote nchini,enyi mnaozitii amri zake.Tafuteni uadilifu, tafuteni unyenyekevu;labda mtaiepa siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
4. Mji wa Gaza utahamwa,Ashkeloni utakuwa tupu.Wakazi wa Ashdodi watatimuliwa mchana,na wale wa Ekroni watang'olewa.
5. Ole wenu wakazi wa nchi za pwani,watu mnaoishi huko Krete!Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenuenyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia:Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!