Nehemia 9:5-11 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Walawi, yaani: Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabuea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakawaambia watu;“Simameni na kumsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.Msifuni milele na milele!Na watu walisifu jina lako tukufu,ambalo hutukuka kuliko baraka na sifa zote.”

6. Ezra akaomba kwa sala ifuatayo:“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu;ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,dunia na vyote vilivyomo,bahari na vyote vilivyomo;nawe ndiwe unayevihifadhi hai,na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.

7. Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu,Mungu uliyemchagua Abramu,ukamtoa toka Uri ya Wakaldayona kumpa jina Abrahamu.

8. Ukamwona kuwa yu mwadilifu mbele yako;ukafanya agano naye kuwapa wazawa wake nchi ya Wakanaani,Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi.Na ahadi yako ukaitimiza;kwani wewe u mwaminifu.

9. “Uliyaona mateso ya babu zetuwalipokuwa nchini Misri,na walipokuomba msaada kwenye Bahari ya Shamuuliwasikia.

10. Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao,watumishi wake wotena watu wote wa nchi yake;kwani ulijua kuwawaliwakandamiza babu zetu.Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.

11. Uliigawa bahari katikati mbele yao,nao wakapita katikati ya bahari,mahali pakavu.Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatiakama jiwe zito ndani ya maji mengi.

Nehemia 9