Mika 3:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu,naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma.

11. Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa,makuhani wake hufundisha kwa malipo,manabii hutabiri kwa fedha.Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu,wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi?Hatutapatwa na madhara yoyote!”

12. Haya! Kwa sababu yenu,Siyoni utalimwa kama shamba,Yerusalemu utakuwa magofu,nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.

Mika 3