Mika 1:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Sanamu zake zote zitavunjwavunjwa,kila kilichochumwa kitateketezwa kwa moto.Vinyago vyake vyote nitaviharibu.Vilirundikwa kutokana na ujira wa malaya,navyo vitatumiwa tena kulipia umalaya.”

8. Kwa sababu hiyo, mimi nitalia na kuomboleza;nitatembea uchi na bila viatu.Nitaomboleza na kulia kama mbweha,nitasikitika na kulia kama mbuni.

9. Majeraha ya Samaria hayaponyeki,nayo yameipata pia Yuda;yamefikia lango la Yerusalemu,mahali wanapokaa watu wangu.

10. Msiitangaze habari hii huko Gathi,wala msilie machozi!Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni.

11. Nendeni enyi wakazi wa Shafiri,mkiwa uchi na wenye haya.Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu.Watu wa Beth-ezeli wanalia;msaada wao kwenu umeondolewa.

12. Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa,lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungukaribu kabisa na lango la Yerusalemu.

Mika 1