Methali 9:4-14 Biblia Habari Njema (BHN)

4. “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:

5. “Njoo ukale chakula,na unywe divai niliyotengeneza.

6. Achana na ujinga upate kuishi;fuata njia ya akili.”

7. Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi,amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa.

8. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia;mwonye mwenye hekima naye atakupenda.

9. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima;mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.

10. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima;na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.

11. Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa;utaongezewa miaka mingi maishani mwako.

12. Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe;kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.

13. Mwanamke mpumbavu ana kelele,hajui kitu wala hana haya.

14. Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake,huweka kiti chake mahali pa juu mjini,

Methali 9