Methali 9:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake,huweka kiti chake mahali pa juu mjini,

15. na kuwaita watu wapitao njiani,watu wanaokwenda kwenye shughuli zao:

16. “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:

17. “Maji ya wizi ni matamu sana;mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.”

18. Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu,wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.

Methali 9