1. Hekima amejenga nyumba yake,nyumba yenye nguzo saba.
2. Amechinja wanyama wa karamu,divai yake ameitayarisha,ametandika meza yake.
3. Amewatuma watumishi wake wa kike mjini,waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko:
4. “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
5. “Njoo ukale chakula,na unywe divai niliyotengeneza.
6. Achana na ujinga upate kuishi;fuata njia ya akili.”
7. Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi,amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa.
8. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia;mwonye mwenye hekima naye atakupenda.
9. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima;mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.