Methali 11:6-14 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Uadilifu wa wanyofu huwaokoa na hatari,lakini wafitini hunaswa kwa tamaa zao wenyewe.

7. Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka;tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu.

8. Mtu mnyofu huokolewa katika shida,na mwovu huingia humo badala yake.

9. Asiyemcha Mungu huangamiza wengine kwa mdomo wake,lakini mwadilifu huokolewa kwa maarifa yake.

10. Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia,na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.

11. Mji hufanikishwa kwa baraka za wanyofu,lakini huangamizwa kwa mdomo wa waovu.

12. Anayemdharau jirani yake hana akili,mtu mwenye busara hukaa kimya.

13. Apitapitaye akichongea hutoa siri,lakini anayeaminika rohoni huficha siri.

14. Pasipo na uongozi taifa huanguka,penye washauri wengi pana usalama.

Methali 11