Maombolezo 3:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Ingawa naita na kulilia msaadaanaizuia sala yangu isimfikie.

9. Njia zangu ameziziba kwa mawe makubwaamevipotosha vichochoro vyangu.

10. Yeye ni kama dubu anayenivizia;ni kama simba aliyejificha.

11. Alinifukuza njiani mwangu,akanilemaza na kuniacha mkiwa.

Maombolezo 3