56. Wewe umenisikia nikikulilia:‘Usiache kusikia kilio changu cha msaadabali unipatie nafuu.’
57. Nilipokuita ulinijia karibuukaniambia, ‘Usiogope!’
58. “Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu,umeyakomboa maisha yangu.
59. Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu,uniamulie kwa wema kisa changu.
60. Umeuona uovu wa maadui zangu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.
61. “Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.