20. Nayafikiria hayo daima,nayo roho yangu imejaa majonzi.
21. Lakini nakumbuka jambo hili moja,nami ninalo tumaini:
22. Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi,huruma zake hazina mwisho.
23. Kila kunapokucha ni mpya kabisa,uaminifu wake ni mkuu mno.
24. Mwenyezi-Mungu ndiye hazina yanguhivyo nitamwekea tumaini langu.
25. Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wanaomtegemea,ni mwema kwa wote wanaomtafuta.
26. Ni vema mtu kungojea kwa saburiukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu.
27. Ni vema mtu kujifunza uvumilivutangu wakati wa ujana wake.
28. Heri kukaa peke na kimya,mazito yanapompata kutoka kwa Mungu.