Maombolezo 3:10-19 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Yeye ni kama dubu anayenivizia;ni kama simba aliyejificha.

11. Alinifukuza njiani mwangu,akanilemaza na kuniacha mkiwa.

12. Aliuvuta upinde wake,akanilenga mshale wake.

13. Alinichoma moyoni kwa mishale,kutoka katika podo lake.

14. Nimekuwa kitu cha dhihaka kwa watu wote,mchana kutwa nimekuwa mtu wa kuzomewa.

15. Amenijaza taabu,akanishibisha uchungu.

16. Amenisagisha meno katika mawe,akanifanya nigaegae majivuni.

17. Moyo wangu haujui tena amani,kwangu furaha ni kitu kigeni.

18. Nimewaza “Nimekata tamaa kabisa,tumaini langu kwa Mwenyezi-Mungu limetoweka.”

19. Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangukwanipa uchungu kama wa nyongo.

Maombolezo 3