12. hakikisheni kwamba hamtamsahau Mwenyezi-Mungu aliyewatoa Misri ambako mlikuwa watumwa.
13. Mtamcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtamtumikia yeye peke yake na kuapa kwa jina lake peke yake.
14. Msiabudu miungu mingine, miungu ya watu walio jirani nanyi,
15. hasira ya Mwenyezi-Mungu isije ikawaka juu yenu, naye akawafutilia mbali kutoka duniani, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliye kati yenu, ni Mungu mwenye wivu.
16. āMsimjaribu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu kule Masa.