Kumbukumbu La Sheria 5:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mose aliwaita pamoja Waisraeli, akawaambia: “Enyi Waisraeli, sikilizeni masharti na maagizo ambayo ninayatamka mbele yenu leo. Jifunzeni hayo na kuyatekeleza kwa uangalifu.

2. Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alifanya agano nasi mlimani Horebu.

3. Hakufanya agano hilo na wazee wetu tu, bali alifanya na sisi sote ambao tuko hai hivi leo.

4. Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi ana kwa ana huko mlimani katikati ya moto.

5. Wakati huo mimi nilisimama kati yenu na Mwenyezi-Mungu, nikawatangazieni yale aliyoyasema, kwa kuwa nyinyi mliogopa ule moto na hamkupanda mlimani. Mwenyezi-Mungu alisema hivi,

6. “ ‘Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri, ambako ulikuwa mtumwa.

7. “ ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.

8. “ ‘Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

Kumbukumbu La Sheria 5