7. Kumbukeni siku zilizopita,fikirieni miaka ya vizazi vingi;waulizeni baba zenu nao watawajulisha,waulizeni wakubwa wenu nao watawaeleza.
8. Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao,alipowagawa wanadamu,kila taifa alilipatia mipaka yake,
9. kulingana na idadi ya watoto wa Mungu,lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake,hao alijichagulia kuwa mali yake.
10. Aliwakuta katika nchi ya jangwa,nyika tupu zenye upepo mkali.Aliwalinda na kuwatunza,aliwafanya kama mboni ya jicho lake.