Kumbukumbu La Sheria 21:18-23 Biblia Habari Njema (BHN)

18. “Kama mtu ana mtoto mkaidi na mtundu, asiyemtii baba yake au mama yake wanapompa nidhamu,

19. basi, mama na baba yake huyo mtoto watamchukua mlangoni mwa nyumba anamoishi na kumpeleka kwa wazee katika lango la mji.

20. Wazazi hao watawaambia wazee wa mji: ‘Mtoto wetu ni mkaidi na mtundu, hataki kutusikiliza, ni mlafi na mlevi.’

21. Hapo watu wa mji huo watampiga mawe mtoto huyo mpaka afe. Ndivyo mtakavyokomesha ubaya huo miongoni mwenu. Kila mtu katika Israeli atasikia tukio hilo na kuogopa.

22. “Kama mtu amefanya kosa la jinai linalompasa auawe na akauawa kwa kutundikwa mtini,

23. maiti yake isiachwe mtini usiku wote, bali mtaizika siku hiyohiyo. Maana mtu aliyenyongwa amelaaniwa na Mungu nanyi hamtaitia najisi nchi yenu mliyopewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, iwe mali yenu.

Kumbukumbu La Sheria 21