Kumbukumbu La Sheria 15:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Lakini mnyama huyo akiwa na dosari yoyote, yaani akiwa kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote kubwa, usimtoe kuwa sadaka kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.

22. Utamla mnyama wa namna hiyo ukiwa katika mji wako; pia wote walio safi na wasio safi wanaweza kumla kama unavyokula paa au kulungu.

23. Lakini usile damu yake; bali hiyo utaimwaga chini kama maji.

Kumbukumbu La Sheria 15