9. “Mnaweza kula kila aina ya samaki wenye mapezi na magamba.
10. Lakini kiumbe chochote kinachoishi majini kisicho na mapezi wala magamba msile; hivyo ni najisi kwenu.
11. “Mnaweza kula ndege wote walio safi.
12. Lakini msile ndege wafuatao: Furukombe, kipungu,
13. kengewa, kozi, mwewe kwa aina zake,
14. kunguru kwa aina zake,
15. mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga kwa aina zake,
16. bundi, mumbi, bundi mkubwa,
17. mwari, nderi, mnandi,
18. membe, koikoi kwa aina zake, hudihudi na popo.
19. Na wadudu wote wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.
20. Mnaweza kula viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi.