Isaya 62:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu;kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.

4. Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”,wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”.Bali utaitwa: “Namfurahia,”na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.”Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe,naye atakuwa kama mume wa nchi yako.

5. Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana,ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako.Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi,ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako.

6. “Juu ya kuta zako ee Yerusalemu nimeweka walinzi,usiku na mchana kamwe hawatakaa kimya.”Enyi mnaomkumbusha Mwenyezi-Mungu ahadi yake,msikae kimya;

7. msimpe hata nafasi ya kupumzika,mpaka atakapousimika mji wa Yerusalemu,na kuufanya uwe fahari ulimwenguni kote.

Isaya 62