2. na juu yake walikuwa wamekaa malaika. Kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Mawili ya kufunika uso, mawili ya kufunika mwili na mawili ya kurukia.
3. Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi:“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu,ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi!Dunia yote imejaa utukufu wake.”
4. Sauti yao iliitikisa misingi ya milango ya hekalu, nalo likajaa moshi.
5. Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
6. Basi, mmoja wa hao malaika akaruka kunijia, akiwa ameshika mkononi koleo lililokuwa na kaa la moto alilolitwaa madhabahuni.
7. Naye akinigusa nalo mdomoni, akasema: “Tazama, kaa hili limekugusa mdomo; umeondolewa hatia yako, umesamehewa dhambi yako.”
8. Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi.”
9. Naye akaniambia, “Nenda ukawaambie watu hawa:‘Mtasikiliza sana, lakini hamtaelewa;mtatazama sana, lakini hamtaona.’”