1. Msifikiri mkono wa Mungu ni mfupi,hata asiweze kuwaokoeni;au masikio yake yamezibika,hata asiweze kuwasikieni.
2. Dhambi zenu ndizo zinazowatenga na Mungu wenu,dhambi zenu zimemfanya ajifiche mbali nanyihata asiweze kuwasikieni.
3. Maana mikono yenu imetiwa najisi kwa mauaji,na vidole vyenu kwa matendo maovu.Midomo yenu imesema uongo,na ndimi zenu husema uovu.