1. Mtu mwadilifu akifa,hakuna mtu anayejali;mtu mwema akifariki,hakuna mtu anayefikiri na kusema:“Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa,
2. ili apate kuingia kwenye amani.”Watu wanaofuata njia ya haki,watakuwa na amani na kupumzika.
3. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Njoni hapa nyinyi wana wa wachawi;nyinyi wazawa wa wachawi, wazinzi na malaya.
4. Je, mnadhani mnamdhihaki nani?Mnamfyonya nani na kumtolea ulimi?Nyinyi wenyewe ni wahalifu tangu mwanzo,nyinyi ni kizazi kidanganyifu.
5. Nyinyi mnawaka tamaa kwenye miti ya mialoni,na katika kila mti wa majani mabichi.Mnawachinja watoto wenuna kuwatambika katika mabonde na nyufa za majabali.
6. Mnachagua mawe laini mabondeni,na kuyafanya kitovu cha maisha yenu.Mnayamiminia tambiko ya kinywajina kuyapelekea tambiko ya nafaka!Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
7. Mmeweka vitanda vyenu juu ya milima mikubwa,na kwenda huko kutoa tambiko.
8. Nyuma ya milango na miimommetundika kinyago chenu.Nyinyi mnaniacha mimina kutandika na kuvipanua vitanda vyenu.Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao.Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya,huku mnakodolea macho kinyago chenu.