Isaya 55:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Haya! Kila mwenye kiu na aje kwenye maji!Njoni, nyote hata msio na fedha;nunueni ngano mkale,nunueni divai na maziwa.Bila fedha, bila gharama!

2. Mbona mnatumia fedha yenukwa ajili ya kitu kisicho chakula?Ya nini kutoa jasho lenu kwa kitu kisichoshibisha?Nisikilizeni mimi kwa makini,nanyi mtakula vilivyo bora,na kufurahia vinono.

3. “Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu;nisikilizeni, ili mpate kuishi.Nami nitafanya nanyi agano la milele;nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi.

Isaya 55