Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Imba kwa shangwe ewe uliye tasa,wewe ambaye hujapata kuzaa!Paza sauti na kuimba kwa nguvu,wewe usiyepata kujifungua mtoto.Maana watoto wako wewe uliyeachwawatakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.