Isaya 46:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Wewe Beli umeanguka;Nebo umeporomoka.Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu.Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama,hao wanyama wachovu wamelemewa.

2. Nyinyi mmeanguka na kuvunjika,hamwezi kuviokoa vinyago vyenu;nyinyi wenyewe pia mtapelekwa uhamishoni!

3. “Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo,nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli.Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa;niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.

4. Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu;hata katika uzee wenu mimi nitawabeba.Nilifanya hivyo kwanza,nitafanya hivyo tena.Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.

5. “Mtanifananisha na nani, tufanane?Je, mwaweza kunilinganisha na nani, tulingane?

Isaya 46