Isaya 42:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza;mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye.Nimeiweka roho yangu juu yake,naye atayaletea mataifa haki.

2. Hatalia wala hatapiga kelele,wala hatapaza sauti yake barabarani.

3. Mwanzi uliochubuka hatauvunja,utambi ufukao moshi hatauzima;ataleta haki kwa uaminifu.

4. Yeye hatafifia wala kufa moyo,hata atakapoimarisha haki duniani.Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.”

5. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungualiyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema,yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo,yeye awapaye watu waliomo pumzi,na kuwajalia uhai wote waishio humo:

Isaya 42