Isaya 41:18-24 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu,na chemchemi katika mabonde.Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji,na nchi kame kuwa chemchemi za maji.

19. Nitapanda miti huko nyikani:Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni;nitaweka huko jangwani:Miberoshi, mivinje na misonobari.

20. Watu wataona jambo hilo,nao watatambua na kuelewa kwambamimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo,mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”

21. Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema:“Enyi miungu ya mataifa,njoni mtoe hoja zenu!

22. Leteni hoja zenu, mtuambie yatakayotukia.Tuambieni matukio ya kwanza yalikuwa yapinasi tutayatafakari moyoni.Au tutangazieni yajayo,tujue yatakayokuja.

23. Tuambieni yatakayotokea baadaye,nasi tujue basi kama nyinyi ni miungu.Fanyeni kitu chochote, chema au kibaya,ili tutishike na kuogopa.

24. Hakika, nyinyi si kitu kabisa.hamwezi kufanya chochote kile.Anayechagua kuwaabudu nyinyi ni chukizo.

Isaya 41